Rehema: Kipawa cha Uadui

101A-001

August 1, 2017

Baba Wa Rehema (1/2)
http://tgvs.org/archives/2870


REHEMA: KIPAWA CHA UADUI
101A-001
Fungu Kuu: Mwanzo 3:15
Muundo: Sauti (Hubiri fupi)

“Nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino.” (Mwanzo 3:15)

Kipawa cha "uadui" dhidi ya Shetani kimetolewa kwa ajili ya wafuasi wote wa Kristo. "Hii "injili ya kwanza"ni unabii wa mapambano na matokeo yake kati ya"uzao wako"(Shetani na wasioamini, ambao wanaitwa watoto wa Ibilisi katika Yohana 8:44) na uzao wake (Kristo, uzao wa hawa, na wale walio katika Yeye), ulioanza bustanini. Katikati ya aya hii ya laana, ujumbe wa matumaini uling'aa mbele---uzao wa mwanamke unaoitwa "Yeye" ni Kristo, ambaye siku moja atamshinda nyoka. Shetani angeweza tu “kuponda kisigino” cha Kristo (kusababisha kuteseka kwake), wakati Kristo ange- “ponda kichwa” cha Shetani (kumwangamiza kwa pigo la kuuwa). " MacArthur kujifunza Biblia.


TUFANYE NINI BASI?

Kata shauri leo kuwa na uadui na “matendo yote ya mwili”.

[1] Uadui na uasherati
[2] Uadui na uchafu
[3] Uadui na ufisadi
[4] Uadui na ibada ya sanamu
[5] Uadui na uchawi
[6] Uadui na uadui, ugomvi, wivu, hasira,
[7] Uadui na fitina, faraka, uzushi,
[8] Uadui na husuda, ulevi, ulafi.
[9] Lakini zaidi sana: Uadui na Shetani.

“Bali wewe, mtu wa Mungu, uyakimbie mambo hayo; ukafuate haki, utauwa, imani, upendo, saburi, upole. Piga vita vile vizuri vya imani; shika uzima ule wa milele ulioitiwa, ukaungama maungamo mazuri mbele ya mashahidi wengi.” (1 Timotheo 6:11-12)



SAUTI YA INJILI
(Hebu sikia sauti (ahadi) ya Bwana tunapofunga kipindi hiki.

“Naye Mungu wa amani atamseta Shetani chini ya miguu yenu upesi. Neema ya Bwana wetu Yesu Kristo na iwe pamoja nanyi - [Amina.]” (Warumi 16: 20)

BWANA ATUBARIKI SOTE!