BIBLIA: “Soma, Elewa, Shuhudia”
MASOMO KUHUSU TABIA YA MUNGU
(a) http://tgvs.org/archives/2253
(b) 77-003: Ghadhabu / Hasira ya Mungu
(c) Kategoria: Mungu
(d) Fungu Kuu: Ebr 10:31
Ebr 10:31 “Ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai.”
OMBI: Baba yetu na Mungu wetu, Jina Lalo litukuzwe. Tunakushukuru kwa nafasi nyingine ya uhai siku hii ya leo. Tunapoenda kutafakari Neno Lako, tunaomba Roho Wako akapate kutufundisha saa hii. Tusamehe dhambi, uovu, makosa na kasoro zetu zote. Tuandaye kwa ajili ya Ufalme Wako. Bariki kila mmoja atakayepata somo hili. Asante Bwana, na twaja katika Jina la Yesu Kristo – Bwana wetu, Amina.
Somo: GHADHABU / HASIRA YA MUNGU
Muhtasari wa Mawazo Makuu.
ASILI YA HASIRA YA MUNGU
(a) Ni ya kuogofya
(b) Ni ya kusita na si ya muda mrefu
(c) Ni sambamba na tabia Yake ya haki na huruma
(d) Inatimiza madhumuni ya Mungu
SABABU ZA HASIRA YA MUNGU
(a) Ibada ya sanamu
(b) kutoamini
(c) Kutotii
(d) Kuvunja Sheria Zake
(e) Maisha yasiyomcha Mungu
(f) Kiburi, Majivuno na Unafiki
(g) Dhuluma
(h) Ukataaji wa watumishi wa Mungu
(i) Malalamiko dhidi ya, na upinzani kwa, madhumuni ya Mungu
JE, MUNGU ANADHIHIRISHAJE HASIRA YAKE?
(a) Nyakati zilizopita
(b) Nyakati za sasa
(c) Nyakati zijazo: "siku ya ghadhabu"
MATOKEO YA HASIRA YA MUNGU
(a) Mungu huruhusu wanaokataa haki kudumu katika dhambi zao
(b) Adhabu ya uhamishoni (Exile)
(c) Adhabu ya Uharibifu wa taifa lote la Israeli
(d) Adhabu kali itatolewa kwao (Waasi)
(e) Adhabu ya kifo
HITIMISHO
(a) Tufanye nini basi?
(b) Sauti Ya Injili kwako
(c) Mwitikio wetu
(d) Ombi la Mwisho
UTANGULIZI: Ghadhabu / Hasira ya Mungu
Ghadhabu / Hasira ya Mungu ni dhana inayotumiwa katika Biblia, ikialika wasomaji wafikirie Hasira ya Mungu inavyotofautishwa na rehema Yake. Kwa asili kabisa Mungu ni mwenye Upendo na Rehema nyingi; lakini pia, anahuzunishwa sna na dhambi. Dhambi ni kinyume cha Tabia Yake (Utakatifu). Wanadamu anapompinga Mungu wake kwa kumdharau, kumkataa, na kuvunja Amri Zake; matokeo yake ni kwamba ghadhabu ya hasira ya Mungu inamwagwa juu yake. “Ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai”. Habari njema ni kwamba mwanadamu anapojirudi na kutubu, Mungu yu radhi kumsamehe. Ni ombi langu kuwa Roho Mtakatifu anapokufundisha somo hili, utajihoji nafsi, utatubu, na kumrudie Mungu wako.
I. ASILI YA HASIRA YA MUNGU
(a) Ni ya kuogofya
Hesabu 1:6
Ni nani awezaye kusimama mbele za ghadhabu yake, naye ni nani awezaye kukaa katika ukali wa hasira yake? Hasira yake kali humwagwa kama moto, nayo majabali yapasuliwa na yeye.
(b) Ni ya kusita na si ya muda mrefu
Kutoka 34:6
Bwana akapita mbele yake, akatangaza, Bwana, Bwana, Mungu mwingi wa huruma, mwenye fadhili, si mwepesi wa hasira, mwingi wa rehema na kweli
(c) Ni sambamba na tabia Yake ya Haki na Huruma
Zaburi 7:11
Mungu ni mwamuzi mwenye haki, Naam, Mungu aghadhibikaye kila siku
Habakuki 3:2
Ee Bwana, nimesikia habari zako, nami naogopa; Ee Bwana, fufua kazi yako katikati ya miaka; Katikati ya miaka tangaza habari yake; Katika ghadhabu kumbuka rehema
(d) Inatimiza madhumuni ya Mungu
Yeremia 30:24
Hasira kali ya Bwana haitarudi, hata atakapokwisha kutenda, hata atakapokwisha kuyatimiza makusudi ya moyo wake; katika siku za mwisho mtayafahamu haya.
II. SABABU ZA HASIRA YA MUNGU
(a) Ibada ya sanamu
Hesabu 25:3
Ikawa Israeli kujiungamanisha na Baal-peori; hasira za Bwana zikawaka juu ya Israeli.
(b) Kutoamini
Yohana 3:36
Amwaminiye Mwana yuna uzima wa milele; asiyemwamini Mwana hataona uzima, bali ghadhabu ya Mungu inamkalia.
(c) Kutotii
Isaya 1:19-20
19 Kama mkikubali na kutii mtakula mema ya nchi; 20 Bali kama mkikataa na kuasi mtaangamizwa kwa upanga; maana kinywa cha Bwana kimenena haya.
(d) Kuvunja Sheria Zake
Ufunuo 21:8
Bali waoga, na wasioamini, na wachukizao, na wauaji, na wazinzi, na wachawi, na hao waabuduo sanamu, na waongo wote, sehemu yao ni katika lile ziwa liwakalo moto na kiberiti. Hii ndiyo mauti ya pili.
(e) Maisha yasiyomcha Mungu
Yuda 1:14b-15
14b Angalia, Bwana alikuja na watakatifu wake, maelfu maelfu, 15 Ili afanye hukumu juu ya watu wote, na kuwaadhibisha wote wasiomcha Mungu, kwa ajili ya kazi zao zote za upotevu walizozitenda bila kumcha Mungu, na kwa ajili ya maneno magumu yote ambayo hao wenye dhambi wasiomcha Mungu wameyanena juu yake.
(f) Kiburi, Majivuno na Unafiki
Mifano mitatu:
1. Mafarisayo (Matayo 23:27-28)
2. Hezekia (2Nyakati 32:25)
3. Efraimu (Hos 12:14)
Mithali 3:34;
Hakika yake huwadharau wenye dharau, Bali huwapa wanyenyekevu neema.
Mithali 8:13;
Kumcha Bwana ni kuchukia uovu; Kiburi na majivuno, na njia mbovu, Na kinywa cha ukaidi pia nakichukia
Isaya 13:11
Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali;
Malaki 4:1
Kwa maana, angalieni, siku ile inakuja, inawaka kama tanuru; na watu wote wenye kiburi, nao wote watendao uovu, watakuwa makapi; na siku ile inayokuja itawateketeza, asema Bwana wa majeshi; hata haitawaachia shina wala tawi.
(g) Dhuluma
Yeremia 22:13
Ole wake aijengaye nyumba yake kwa uovu! Na vyumba vyake kwa udhalimu! Atumiaye utumishi wa mwenzake bila ujira, Wala hampi mshahara wake
Mal 3:5
Nami nitawakaribieni ili kuhukumu; Nami nitakuwa shahidi mwepesi juu ya wachawi, na juu ya wazinzi, na juu yao waapao kwa uongo; na juu yao wamwoneao mwenye kuajiriwa, kwa ajili ya mshahara wake, wamwoneao mjane na yatima, na kumpotosha mgeni asipate haki yake, wala hawaniogopi mimi, asema Bwana wa majeshi.
(h) Ukataaji wa “Mtumishi”; au watumishi wa Mungu
Waebrania 10:29-31
29 Mwaonaje? Haikumpasa adhabu iliyo kubwa zaidi mtu yule aliyemkanyaga Mwana wa Mungu, na kuihesabu damu ya agano aliyotakaswa kwayo kuwa ni kitu ovyo, na kumfanyia jeuri Roho wa neema? 30 Maana twamjua Yeye aliyesema, Kupatiliza kisasi ni juu Yangu, Mimi nitalipa. Na tena, Bwana atawahukumu watu wake. 31 Ni jambo la kutisha kuanguka katika mikono ya Mungu aliye hai.
(i) Malalamiko/ Upinzani dhidi ya mapenzi ya Mungu
Hesabu 11:1
Kisha hao watu walikuwa kama wanung'unikao, wakinena maovu masikioni mwa Bwana; Bwana aliposikia hayo, hasira zake zikawaka; na moto wa Bwana ukawaka kati yao, ukateketeza katika mipaka ya mwisho wa marago
Hesabu 21:5
5 Watu wakamnung'unikia Mungu, na Musa, Mbona mmetupandisha huku kutoka nchi ya Misri, ili tufe jangwani? Maana hapana chakula, wala hapana maji, na roho zetu zinakinai chakula hiki dhaifu. 6 Bwana akatuma nyoka za moto kati ya watu, wakawauma, watu wengi wakafa.
(j) Kumdharau Bwana
Danieli 5: 23-30 (Mfalme Belshaza)
23 Bali umejiinua juu ya Bwana wa mbingu; nao wamevileta vyombo vya nyumba yake mbele yako; na wewe, na wakuu wako, na wake zako, na masuria wako, mmevinywea; nawe umeisifu miungu ya fedha na ya dhahabu na ya shaba, na ya chuma, na ya mti, na ya mawe; wasioona, wala kusikia, wala kujua neno lo lote; na Mungu yule, ambaye pumzi yako i mkononi mwake, na njia zako zote ni zake, hukumtukuza.
24 Ndipo kile kitanga cha ule mkono kikaletwa kutoka mbele zake, na maandiko haya yameandikwa.
25 Na maandiko yaliyoandikwa ni haya; MENE, MENE, TEKELI, NA PERESI.
26 Na tafsiri ya maneno haya ni hii; MENE, Mungu ameuhesabu ufalme wako na kuukomesha.
27 TEKELI, umepimwa katika mizani nawe umeonekana kuwa umepunguka.
28 PERESI, ufalme wako umegawanyika, nao wamepewa Wamedi na Waajemi.
29 Ndipo Belshaza akatoa amri, nao wakamvika Danielii mavazi ya rangi ya zambarau, wakatia mkufu wa dhahabu shingoni mwake, wakapiga mbiu kutangaza habari zake, ya kwamba yeye ni mtu wa tatu katika ufalme.
30 Usiku uo huo Belshaza, mfalme wa Wakaldayo, akauawa.
(k) Kumdanganya Mungu
Matendo 5:1-10 (Anania & Safira)
1 Lakini mtu mmoja jina lake Anania, pamoja na Safira mkewe, aliuza mali, 2 Akazuia kwa siri sehemu ya thamani yake, mkewe naye akijua haya, akaleta fungu moja akaliweka miguuni pa mitume. 3 Petro akasema, Anania, kwa nini Shetani amekujaza moyo wako kumwambia uongo Roho Mtakatifu, na kuzuia kwa siri sehemu ya thamani ya kiwanja? 4 Kilipokuwa kwako, hakikuwa mali yako? Na kilipokuwa kimekwisha kuuzwa, thamani yake haikuwa katika uwezo wako? Ilikuwaje hata ukaweka neno hili moyoni mwako? Hukumwambia uongo mwanadamu, bali Mungu.
5 Anania aliposikia maneno haya akaanguka, akafa. Hofu nyingi ikawapata watu wote walioyasikia haya. 6 Vijana wakaondoka, wakamtia katika sanda, wakamchukua nje, wakamzika.
7 Hata muda wa saa tatu baadaye mkewe akaingia, naye hana habari ya hayo yaliyotokea. 8 Petro akamjibu, Niambie, Mlikiuza kiwanja kwa thamani hiyo? Akasema, Ndiyo, kwa thamani hiyo. 9 Petro akamwambia, Imekuwaje hata mkapatana kumjaribu Roho wa Bwana? Angalia, miguu yao waliomzika mumeo ipo mlangoni, nao watakuchukua nje wewe nawe.
10 Mara akaanguka miguuni pake akafa; wale vijana wakaingia wakamkuta amekufa, wakamchukua nje, wakamzika pamoja na mumewe.
JE, MUNGU ANADHIHIRISHAJE HASIRA YAKE?
Yeremia 10:10
(a) Nyakati zilizopita (mfano: Isaraeli)
Hesabu 14:27
27 Je! Nichukuane na mkutano mwovu huu uninung'unikiao hata lini? Nimesikia manung'uniko ya wana wa Israeli, waninung'unikiayo 28 Waambieni, Kama niishivyo, asema Bwana, hakika yangu kama ninyi mlivyonena masikioni mwangu, ndivyo nitakavyowafanyia ninyi; 29 mizoga yenu itaanguka katika jangwa hili, na wote waliohesabiwa miongoni mwenu, kama jumla ya hesabu yenu, tangu waliopata umri wa miaka ishirini na zaidi, hao walioninung'unikia, 30 hakika yangu hamtaingia ninyi katika nchi, ambayo niliinua mkono wangu ya kwamba nitawaketisha humo, isipokuwa Kalebu mwana wa Yefune, na Yoshua mwana wa Nuni.
(b) Nyakati za sasa
Warumi 1:18
Kwa maana ghadhabu ya Mungu imedhihirishwa kutoka mbinguni juu ya uasi wote na uovu wa wanadamu waipingao kweli kwa uovu.
(c) Nyakati zijazo: "siku ya ghadhabu"
Warumi 2:5-6
5 Bali kwa kadiri ya ugumu wako, na kwa moyo wako usio na toba, wajiwekea akiba ya hasira kwa siku ile ya hasira na ufunuo wa hukumu ya haki ya Mungu, 6 atakayemlipa kila mtu kwa kadiri ya matendo yake.
Isaya 13:9,13;
9 Tazama, siku ya Bwana inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake. 13 Kwa hiyo nitazitetemesha mbingu, na dunia itatikiswa itoke katika mahali pake, kwa sababu ya ghadhabu ya Bwana wa majeshi, na kwa sababu ya siku ya hasira yake kali.
Sefania 1:14-18
14 Hiyo siku ya Bwana iliyo kuu i karibu; I karibu, nayo inafanya haraka sana; Naam, sauti ya siku ya Bwana; Shujaa hulia kwa uchungu mwingi huko!
15 Siku ile ni siku ya ghadhabu, Siku ya fadhaa na dhiki, Siku ya uharibifu na ukiwa, Siku ya giza na utusitusi, Siku ya mawingu na giza kuu,
16 Siku ya tarumbeta na ya kamsa, Juu ya miji yenye maboma, Juu ya buruji zilizo ndefu sana.
17 Nami nitawaletea wanadamu dhiki, hata watakwenda kama vipofu, kwa sababu wamemtenda Bwana dhambi; na damu yao itamwagwa kama mavumbi, na nyama yao kama mavi.
18 Fedha yao wala dhahabu yao havitaweza kuwaokoa katika siku ile ya ghadhabu ya Bwana; bali nchi yote pia itateketezwa kwa moto wa wivu wake; maana atawakomesha watu wote wakaao katika nchi hii, naam, ukomo wa kutisha.
MATOKEO YA HASIRA YA MUNGU
Mungu huruhusu wanaokataa haki kudumu katika dhambi zao
2 Nyakati 12:5b
Bwana asema hivi, Ninyi mmeniacha Mimi, kwa hiyo Nami nimewaacha ninyi mkononi mwa Shishaki.
Nehemia 9:28;
Lakini walipokuwa wamekwisha kustarehe, walitenda mabaya tena mbele zako; kwa hiyo ukawaacha katika mikono ya adui zao, nao wakawatawala; hata hivyo waliporejea na kukulilia, uliwasikia toka mbinguni; ukawaokoa mara nyingi kwa rehema Zako;
Isaya 54:7-8;
7 Kwa kitambo kidogo nimekuacha; lakini kwa rehema nyingi nitakukusanya.
8 Kwa ghadhabu ifurikayo nalikuficha uso wangu dakika moja; lakini kwa fadhili za milele nitakurehemu, asema Bwana, Mkombozi wako.
Adhabu ya uhamishoni (Exile)
1 Wafalme 14:15
Kwa kuwa Bwana atawapiga Israeli kama manyasi yatikiswavyo majini; naye atawang'oa Israeli katika nchi hii njema, aliyowapa baba zao, naye atawatawanya ng'ambo ya Mto; kwa sababu wamejifanyia maashera yao, wakimkasirisha Bwana.
Adhabu ya Uharibifu wa taifa lote la Israeli
Ezekieli 38:19-22
19 Kwa maana katika wivu wangu, na katika moto wa ghadhabu yangu, nimenena, Hakika katika siku ile kutakuwako tetemeko kubwa katika nchi ya Israeli;
20 hata samaki wa baharini, na ndege wa angani, na wanyama wa kondeni, na vitu vyote vitambaavyo juu ya nchi, na wanadamu wote walio juu ya uso wa nchi, watatetemeka mbele ya uso wangu; nayo milima itatupwa chini, na magenge yataanguka, na kila ukuta utaanguka chini.
21 Nami nitaita upanga, uje juu yake katika milima yangu yote, asema Bwana MUNGU; nao upanga wa kila mtu utakuwa juu ya ndugu yake.
22 Nami nitamhukumu kwa tauni, na kwa damu; nami nitanyesha mvua ifurikayo, na mvua ya mawe makubwa sana, na moto na kiberiti juu yake, na vikosi vyake, na watu wa kabila nyingi walio pamoja naye.
Adhabu kali itatolewa kwao (Waasi)
2 Petro 3:6-7
6 Kwa hayo dunia ile ya wakati ule iligharikishwa na maji, ikaangamia.
7 Lakini mbingu za sasa na nchi zimewekwa akiba kwa moto, kwa neno lilo hilo, zikilindwa hata siku ya hukumu, na ya kuangamia kwao wanadamu wasiomcha Mungu.
2 Wathesalonike 1:8-9
8 Katika mwali wa moto; huku akiwalipiza kisasi wao wasiomjua Mungu, na wao wasioitii Injili ya Bwana wetu Yesu; 9 Watakaoadhibiwa kwa maangamizi ya milele, kutengwa na uso wa Bwana na utukufu wa nguvu zake;
Adhabu ya kifo
Hesabu 32:13;
Na hasira za Bwana ziliwaka juu ya Israeli, naye akawatembeza huku na huku jangwani muda wa miaka arobaini, hata kizazi hicho kizima kilichokuwa kimefanya uovu machoni pa Bwana kikaisha angamia
Yoshua 7:25-26; (Bonde la Akori)
25 Yoshua akasema, Mbona umetufadhaisha hivi? Bwana atakufadhaisha wewe leo. Ndipo Israeli wote wakampiga kwa mawe, kisha wakawateketeza kwa moto, na kuwapiga kwa mawe.
26 Kisha wakakusanya juu yake chungu kubwa ya mawe hata leo; naye Bwana akauacha ukali wa hasira yake. Kwa sababu hiyo jina la mahali pale likaitwa, Bonde la Akori, hata hivi leo.
Isaya 13:9-13;
9 Tazama, siku ya Bwana inakuja, siku kali, ya hasira na ghadhabu kuu, ili iifanye nchi kuwa ukiwa, na kuwaharibu watu wake, wenye dhambi, wasikae ndani yake.
10 Maana nyota za mbinguni na matangamano havitatoa nuru yake; jua litatiwa giza wakati wa kucha kwake, na mwezi utaacha nuru yake isiangaze.
11 Nami nitaadhibu ulimwengu kwa sababu ya ubaya wake, na wenye dhambi kwa sababu ya hatia yao; nami nitaikomesha fahari yao wenye kiburi; nami nitayaangusha chini majivuno yao walio wakali;
12 Nitafanya wanadamu kuadimika kuliko dhahabu safi, na watu kuliko dhahabu ya Ofiri.
13 Kwa hiyo nitazitetemesha mbingu, na dunia itatikiswa itoke katika mahali pake, kwa sababu ya ghadhabu ya Bwana wa majeshi, na kwa sababu ya siku ya hasira Yake kali.
BAADHI YA MIFANO MINGINE.
(a) Danieli 5:30; (Anania)
(b) Matendo 5:5,10 (Belshaza)
(c) Mwanzo 19 (Sodoma & Gomora)
(d) Waisraeli-Jangwani
(e) Shetani na Malaika zake
TUFANYE NINI BASI?
Injili ya leo inatualika kumpenda Mungu na kuachana na dhambi zilizotajwa:
(a) Ibada ya sanamu
(b) kutoamini
(c) Kutotii
(d) Kuvunja Sheria za Mungu
(e) Maisha yasiyomcha Mungu
(f) Kiburi, Majivuno na Unafiki
(g) Dhuluma
(h) Kumpinga Kristo Yesu
(i) Kuwapuuza/ Kuwapinga watumishi wa Bwana
(j) Malalamiko dhidi ya, na upinzani kwa, madhumuni ya Mungu
TUFANYE NINI BASI?
Tumuombe Mungu atusaidie kumtii na kuzishika Amri Zake, kama zilivyoelezwa katika kitabu cha Kutoka 20.
(1) Usiwe na miungu mingine ila Mimi.
(2) Usijifanyie sanamu ya kuchonga
(3) Usilitaje bure jina la Bwana, Mungu wako
(4) Ikumbuke siku ya Sabato uitakase.
(5) Waheshimu baba yako na mama yako
(6) Usiue.
(7) Usizini.
(8) Usiibe.
(9) Usimshuhudie jirani yako uongo.
(10) Usiitamani
AHADI YA BWANA
Kutoka 20:5-6
5 Usivisujudie wala kuvitumikia; kwa kuwa mimi, Bwana, Mungu wako, ni Mungu mwenye wivu; nawapatiliza wana maovu ya baba zao, hata kizazi cha tatu na cha nne cha wanichukiao, 6 Nami nawarehemu maelfu elfu wanipendao, na kuzishika amri zangu.
HASIRA YA MWANAKONDOO
Ufunuo 6:14-17
14 Mbingu zikaondolewa kama ukurasa ulivyokunjwa, na kila mlima na kisiwa kikahamishwa kutoka mahali pake.
15 Na wafalme wa dunia, na wakuu, na majemadari, na matajiri, na wenye nguvu, na kila mtumwa, na mwungwana, wakajificha katika pango na chini ya miamba ya milima,
16 Wakiiambia milima na miamba, Tuangukieni, tusitirini, mbele za uso wake yeye aketiye juu ya kiti cha enzi, na hasira ya Mwana-Kondoo.
17 Kwa maana siku iliyo kuu, ya hasira yao, imekuja; naye ni nani awezaye kusimama?
SAUTI YA INJILI
Ebu sikia Sauti ya Bwana ikinena nawe leo:
Isaya 44:22.
Nimeyafuta makosa yako kama wingu zito, na dhambi zako kama wingu; unirudie; maana nimekukomboa.
Isaya 1:18
Haya, njoni, tusemezane, asema Bwana. Dhambi zenu zijapokuwa nyekundu sana, zitakuwa nyeupe kama theluji; zijapokuwa nyekundu kama bendera, zitakuwa kama sufu.
MWITIKIO WETU
NZK # 143: “Baba sina Msaada”
1
Baba sina msaada ila kwako pekee,
Kama kwangu ungefichwa, nifanyeje Baba?
Chorus:
Sasa hivi naamini, Yesu alikufa,
Aliimwaga damu yake, nitoke dhambini.
2
Naamini mwana wako, nipe nguvu zako,
Nijazie mahitaji, katika saa hii.
3
Ni furaha gani kwangu, kukuona uso,
Nijue sauti yako, nipate neema.
HITIMISHO
Wapendwa baada ya kutafakari somo hili kwa kina, najikuta kuwa mimi ni mwenye dhambi na ninastahili gadhabu ya Hasira ya Mungu. Lakini, Bwana asifiwe kwa sababu, amenihurumia na kunisamehe. Na sasa anakuita nawe, mpendwa... achana na dhambi zako. Sikia Sauti Yake ikinena nawe kwa upole. Mlango bado u wazi. Nafasi ya Toba bado ipo. Usikawie mpendwa. Fanya hima, mrudie Bwana Mungu wako leo.
OMBI LA MWISHO
Na Bwana twaja tena Kwako tukisema asante sana kwa somo la leo. Asante kwa nafasi nyingine ya Toba unayotupatia siku hadi siku. Asante kwa sababu u tayari kutusamehe dhambi, uovu na makosa yetu, kama inavyoelezwa wazi na mtunga Zaburi , akisema: “1 Ee Bwana, toka vilindini nimekulilia. 2 Bwana, uisikie sauti yangu. Masikio yako na yaisikilize Sauti ya dua zangu. 3 Bwana, kama Wewe ungehesabu maovu, Ee Bwana, nani angesimama? 4 Lakini kwako kuna msamaha, Ili Wewe uogopwe.” (Zaburi 130:1-4). Asante Bwana, kwa sababu “kwako kuna msamaha”
Ee Bwana, “Unisafishe kwa hisopo nami nitakuwa safi, Unioshe, nami nitakuwa mweupe kuliko theluji.” (Zaburi 51:7) Nikumbushe juu ya Upendo wa Mungu, lakini unikumbushe pia juu ya hasira Yake dhidi ya dhambi.
Ee Bwana, saidia mmoja atakaye soma injili ya leo akate shauri na aje Kwako leo. Hebu Roho Wako akaendelee kunena nasi. Na siku ujapo tuweze kuwa miongoni mwa washindani, wale watakao imba na kusema: “Tazama, huyu ndiye Mungu wetu, Ndiye tuliyemngoja atusaidie; Huyu ndiye Bwana tuliyemngoja, Na tushangilie na kuufurahia wokovu wake.” (Isaya 29:9).
Asante Bwana kusikia ombi hili fupi, ni katika Kristo aliye Bwana na Mwokozi wetu, tumeomba, Amina.
The Gospel’s Voice © 2017
Hasira ya Mungu
77-003
February 25, 2017
Share
Facebook
X
Link
https://thegospelsvoice.subspla.sh/7r9jlbm
Copy
Copy this text
Embed code
<div style="position:relative;width:100%;height:0;padding-top:56.25%;"><iframe src="https://subsplash.com/+70f6/embed/mi/+7r9jlbm?info&embeddable&shareable&logo_watermark" frameborder="0" webkitallowfullscreen mozallowfullscreen allowfullscreen style="position:absolute;top:0;left:0;width:100%;height:100%;"></iframe></div>
Copy
Copy this text
Related